Feedback Sitemap Send page Print Help
Mtandao wa waalimu Afrika

Lengo la mradi huu ni kuendesha utafiti kwenye kozi mbalimbali za maendeleo kwenye mtandao unaowalenga waalimu wa Afrika. Lengo kuu la mradi huu ni kuangalia kozi zilizopo  na kuchanganua ujuzi kwenye kozi hizi  za mtandao. Lengo  la mwisho ni kutoa mwongozo  ambao unachanganua kozi ya maendeleo ya  kitaalamu kwa walimu bora.

Malengo:

  • Kuweka msingi wa mawasiliano wa ujuzi kati ya walimu wa Afrika kutoka nchi mbalimbali  kukiwa na uhusiano maalumu na elimu ya ICTs mashuleni.
  • Kuhakikisha kwamba mtandao umeanzishwa ili kuongoza shirika la SchoolNet Africa kwenye uundaji wa bohari la elimu na maarifa Afrika, ambalo kwa upana wake litakuwa linawalenga walimu wa Afrika.
  • Kutoa nafasi kwa walimu wa kiafrika kwa kuwahamasisha kushiriki kwenye makala za kidunia, hivyo kuongeza ushiriki wa Afrika katika makala za dunia.

Mitizamo na Malengo:

Mtazamo wa Mtandao wa waalimu wa Kiafrika (African Teachers Network)  ni kuwa jamii inayojiendesha kwa utaalam wa hali ya juu wa kiafrika uliofuzu katika elimu ya madarasa kwa ajili ya madarasa ya Afrika.

Malengo ya Mtandao wa waalimu wa Kiafrika  ni kuanzisha mtandao imara wa waalimu kutoka shule mbalimbali Afrika ambao wataimarisha uwezo wa elimu kwa wakufunzi wa kiafrika kupitia miradi ya ushirikiano, kuinua  ushiriki kwenye makala za elimu kidunia na mpango wa maendeleo ya kitaalam kwa wakufunzi hivyo kuboresha ufundishaji katika shule za Afrika.