Feedback Sitemap Send page Print Help
Historia yetu

Hii yote ilianza kwenye warsha iliyofanyika mjini Cape Town mwezi wa Septemba, 2020 ambapo ilihudhuriwa na wawakilishi wa SchoolNet kutoka nchi kumi za kiafrika. SchoolNet Africa Case Statement - Tamko la hali ya Afrika ambalo lilikuwa limepangwa kwenye makala ya maendeleo ya uchumi wa Afrika (ADF) iliyodhaminiwa na kamati ya umoja wa mataifa ya maendeleo ya uchumi wa Afrika (UNECA) mwezi November ’99, ilikubaliwa katika warsha hii. ADF kwa utaratibu walikubali jitihada zetu.

Kwa msaada kutoka kituo cha kimataifa cha utafiti wa maendeleo International Development Research Centre (IDRC), mpango wa biashara wa SchoolNet ulioandaliwa na kupangwa kwenye warsha ya mitandao ya shule katika Afrika, iliyofanyika Okahandja, Namibia mwezi July,  2020. Warsha hii ilidhaminiwa na SchoolNet Namibia, Wizara ya elimu nchini Namibia, Taasisi ya Taifa ya maendeleo ya Elimu na IDRC. Warsha hii ilihudhuriwa na wawakilishi zaidi ya 100 kutoka kwenye miradi ya SchoolNet, wiraza za Elimu, mashirika binafsi kutoka nchi ishirini za kiafrika. Wakati huo huo,   kamati ya muda ya uongozi ilichaguliwa ikiwa na wawakilishi wawili kutoka katika kila maeneo matano ya Afrika.

Ripoti ya School Networking in Africa Workshop kwa habari zaidi. 

Mwezi July,  2020 kamati ya uongozi ya muda ilikutana kwa mara ya kwanza huko mjini CapeTown na kuendelea katika maandalizi ya uanzilishi wa SchoolNet Africa kama asasi inayojitegemea ikishirikiana na taasisi ya jamii huru ya kusini mwa Afrika Open Society Institute for Southern Africa (OSISA).

 

Mtizamo wetu

Kumuwezesha mtoto wa kiafrika kuwa msitari wa mbele katika ushiriki wa dunia kupitia matumizi sahihi ya teknolojia na mawasiliano ( ICTs) katika Elimu.

Malengo yetu

  • SchoolNet Africa inasimamia haki zote za vijana wa kiafrika katika elimu na nafasi za mafunzo kwa maisha ya kudumu.
  • SchoolNet Africa inasimamia haki za kila kijana wa kiafrika kuwa na uwazo wa kupata habari
  • Tunasimama kwa mpango endelevu na unaoweza kumudiwa na wote kataka ICT kwa shule za kiafrika.
  • Habari za elimu za kiafrika kwenye mtandao wa kompyuta.
  • Tumafanya kazi kuelekea kwenye uendelezi wa yaliyomo kwenye mtandao kwa kutumia lunga za wenyeji.

Mtandao wetu

SchoolNet Africa inafanya kazi na viongozi wa miradi ya SchoolNet Africa katika nchi 30 za kiafrika. Nchi hizi ni pamoja na;
o Angola
o Benin
o Botswana
o Cameroon
o Cape Verde
o Cote D'lvoire
o Egypt
o Ethiopia
o Gambia
o Ghana
o Kenya
o Lesotho
o Malawi
o Mauritius
o Morocco
o Mozambique
o Namibia
o Nigeria
o Rwanda
o Senegal
o Sierra Leone
o South Africa
o Swaziland
o Tanzania
o Uganda
o Zambia
o Zimbabwe

 

SchoolNet Africa ilizindiliwa rasmi tarehe 12 November 2020 .

Wasiliana nasi

Shirika letu

Bodi yetu ya Uongozi

Wabia