Feedback Sitemap Send page Print Help
Kuunda Mabingwa wa SchoolNet

Lengo kuu la kuunda mabingwa wa SchoolNet barani Afrika ni kuanzisha kundi la viongozi wa kiafrika ambao wamepata ujuzi wa aina mbali mbali kuongoza mabadiliko katika elimu katika ngazi za kitaifa. Mpango huu unajumuisha miradi mbalimbali inayolenga kujenga uwezo wa uongozi kati ya kundi la viongozi chipukizi katika kuinua elimu kupitia ICTs kwa shule za Afrika.

 

Kwa nini mpango wa African SchoolNet Champions?

Kuundwa kwa asasi ya SchoolNet imekuwa ni jibu la kilio cha matumizi sahihi ya ICTs, umuhimu wake kwenye elimu na mtindo wa pekee wa wanafunzi kuendana na mafunzo ya walimu. Kuundwa kwake pia kumeendana na matakwa ya ongezeko la tabaka la maarifa pamoja na umuhimu wa matumizi ya teknolojia katika kuunda mfumo sahihi wa elimu ambao unaweza kusaidia katika elimu ya msingi na  sekondari kidunia

Asasi za SchoolNet katika nchi mbalimbali Afrika zina historia tofauti katika uanzishwaji wake. Baadhi ziliundwa na walimu bingwa wakiongoza njia, nyingine kupitia wafadhili na mawakala wa maendeleo kama kiini, wakati nyingine zilionana na mabingwa ICT wakiangalia ICT kwenye mashule kama njia muhimu kwa maendeleo ya nchi yao.

Katika nchi nyingi za kiafrika, asasi za SchoolNet ziko katika hatua tofauti tofauti za kimaendeleo. Watu walioajiriwa au wanaojitolea kwenye SchoolNet wanakuwa na ujuzi tofauti tofauti. Hata hivyo, asasi bado inakuwa inahitaji uongozi wa elimu na mafunzo kuwawezesha kufanya kazi katika hali ya juu, kuonyesha ufanisi zaidi, uzalishaji wakati wa kutoa huduma na bidhaa kwenye elimu na mfumo wa kurundishia.

Umuhimu huu ulipendekezwa na kuambatanishwa wakati wa warsha inayolenga SchoolNets katika Afrika na ambayo ilipelekea kuundwa kwa kamati ya muda ya SNA. Warsha hii ilifanyika nchini Namibia kuanzia tarene 17-20, July 2020, ilitaka kamati ya muda ya SNA kutafakari maendeleo ya mabingwa wa SNA kama sehemu muhimu kwenye mpango wa utekelezaji.