Feedback Sitemap Send page Print Help
Kusaidia SchoolNet

Lengo la ScholNet Africa ni kusaidia SchoolNet za kitaifa kuweka sawa na kuhamashisha vyanzo. Wakati huo huo, SchoolNet za kitaifa zinasaidia SNA kwa kujiandikisha kama wanachamaa na kuwasaidia SNA kuhusu uzoefu na jinsi wanavyoweza kufanya kazi na kusaidia SchoolNet zingine katika Afrika.

Waanzilishi wa SchoolNet

Kenya SNA inafanya kazi na washiriki nchini Kenya kwenye udadisi wa mazingira na warsha kujadili maendeleo ya SchoolNet nchini humo. Kama ungependa kusaidia wasiliana na Lucy Kinjanjui kupitia barua pepe ifuatayo [email protected]

Malawi

SNA inafanya kazi na washirika wa Malawi ili kupata uwezo wa kompyuta ikishirikiana na computer Aid International. Kama unahamasika kusaidia tafadhali wasiliana na Bessie Nyindera kupitia [email protected]

Mali

SNA inafanya kazi na washirika wa Mali kuendeleza mpango wa biashara wa ScholNet katika kupata nyanzo na kuanzisha SchoolNets. SNA pia inasaidia mafunzo ya walimu nchini  Mali. SNA imefanya kazi na SchoolNet Mali katika kuinua shughuli za Thinkquest Africa.

Msumbiji

SNA inafanya kazi na SchoolNet Msumbiji katika kukendeleza mpango wa biashara na kupata vyanzo vya kuanzisha mafunzo ya walimu

Sudan

SNA imewasiliana na washirika ambao wana nia ya kuanzisha SchoolNet Sudan. Mpango wa kibiashara bado unafanyiwa kazi.

Misaada ilivyo

SchoolNet Cameroon

SchoolNet Cameroon ni mshirika muhimu kitaifa katika SNA. SNA itasaidia kuanzishwa kwa shughuli za SchoolNet Cameroon

SchoolNet Nigeria

SNA ilishiriki kwenye uzinduzi wa SchoolNet Nigeria, September 2020. Toka hapo SNA inesaidia SchoolNet Nigeria kwenye kuendeleza mpango wa ThinkQuest. SNA inasaidia kampeni ya e-rate Nigeria  na kampeni ya ufahamu wa ICTs katika elimu.

SchoolNet South Africa

SNSA ni mshirika wa muda mrefu wa SNA. SNSA ilikuwa ndio chombo cha uanzishaji wa SNA na kihistoria, imesaidia uanzishaji wa SchoolNet Namibia. SNA hivi karibuni wameshirikiana na SNSA katika upatikanaji wa wakufunzi kutoka nchini Uganda ili kuweza kusaidia katika tovuti ya SNSA. SNSA pia inafanya kazi na SNA kwenye Think Quest Africa kwa kuandaa na kusaidia utoaji huduma wa TQA.

Ghana : ushirikiano wa mtandao katika elimu

SNA   inashirikiana na  PIE katika kuhamasisha washika dau kitaifa kuanzisha mpango wa SchoolNet unaounganisha SchooNet zote kitaifa. Kwa habari zaiki wasiliana na Eric Yankah [email protected]

SchoolNet Namibia

 SNA ilishirikiana na SchoolNet Namibia kwenye mradi wa ICTs katika umuhimu maalum wa elimu. SchoolNet  Namibia pia inajihusisha na mradi wa  ThinkQuest Africa. Kwa habari zaidi wasiliana na Joris Komen kupitia; [email protected]