Feedback Sitemap Send page Print Help
Kutoka katika matumizi ya silaha kwenda kwenye kompyuta

Habari na mawasiliano ya kiteknolojia (ICTs)  kama asasi ya kwanza inayoongozwa na Waafrika katika elimu, SchoolNet Africa inaamini kwamba ICTs ni nyenzo za kuharakisha nafasi za Elimu kwa vijana wa Afrika na ina nafasi kubwa ya kufikia elimu katika nyanja zote. Makala hii inaelezea mradi wa majaribio wa kutambulisha mpango wa elimu kupitia habari na mawasiliano ya kiteknolojia (ICTs) kwa wapiganaji watoto walioshiriki vita katika nchi tatu za Afrika; Angola, Liberia na Rwanda.

 

Mradi unatazamia kuanzisha kitovu cha habari za ICT na ufundishaji wa ujuzi kwa watoto waliopigana vita nchini Angola, Liberia na Rwanda.

 

Malengo ya mradi

Kuanzisha upatikanaji wa habari kupitia kompyuta kwa watoto wapiganaji katika miji mitatu nchini  Angola, Liberia na Rwanda.

  1. Kutoa ujuzi wa kompyuta kwa watoto wapiganaji 100 katika kila hizo nchi tatu mpaka kufikia mwisho wa mwaka 2020.
  2. Kutoa ushauri wakisaikolojia kwa watoto waliokuwa wamefunzwa kuwa wapiganaji.
  3. Kusaidia katika kuwabadili tabia watoto waliopigana ili kuingia katika mkondo wa jamii ya familia, elimu na nafasi za kazi.
  4. Kuelezea ushiriki katika mpango wa kitaifa kwa kipimo cha hali ya juu.

Mafanikio na matokeo ya mradi

  1. Miji mitatu ya Angola, Liberia na Rwanda itakuwa imepatiwa mfumo wa kompyuta. Zaidi ya watoto 100 waliopigana vita watakuwa wamefunzwa nadharia na ufundi katika ujuzi wa kompyuta.
  2. Watoto 300 waliopigana watakuwa wamebadilishwa tabia na kufundishwa katika kila nchi mojawapo ili kuweza kuingia kwenye mfumo wa jamii
  3. Muundo, mtandao na vifaa  vitapatikana katika nchi hizo tatu kwa kufunza,
  4. kushauri na kuwarekebisha watoto wengine waliopigana.
  5. Ripoti ya mchanganuo na mwenendo itapatikana ili kuwezesha kufanya mradi kama katika nchi nyingine.

Hitimisho

Kama ilivyo habari ya watoto wapiganaji inaendelea kukwaza elimu kwa malengo yote katika Afrika, SchoolNet Africa inawataka washikadau katika elimu ndani ya Angola, Liberia na Rwanda, Asasi zisizo za kiserikali na jumuiya ya wafadhili wa kitaifa kusaidia mradi huu. Inatumainiwa kwamba, kufanikiwa kwa mradi huu wa majaribio utaongoza kwenye kupanuliwa kwa nafasi za elimu kupitia habari na mawasiliano ya kiteknojolia (ICTs) kwa watoto waliopigana katika nchi nyingine zilizoathirika na vita kama vile; Sierra Lione, Burundi, Sudan, Somalia pamoja na Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.