Feedback Sitemap Send page Print Help
Shirika letu

Kumuwezesha mtoto wa kiafrika kuwa msitari wa mbele katika ushiriki wa dunia kupitia matumiza sahihi ya teknolojia na mawasiliano ( ICTs) katika Elimu.

Malengo yetu:

Lengo letu ni kusaidia SchoolNet kitaifa katika Afrika nzima kwa kuhamasisha wafadhili kujenga ushirika sahihi na maarifa katika kuinua elimu kupitia matumizi endelevu ya ICTs katika shule za kiafrika.

  • SchoolNet Africa inasimamia haki zote za vijana wa kiafrika katika elimu na nafasi za mafunzo kwa maisha ya kudumu.
  • SchoolNet Afrika inasimamia haki za kila kijana wa kiafrika kuwa na uwezo wa kupata habari.
  •  Tunasimama kwa mpango endelevu na unaoweza kumudiwa na wote katika ICT kwa shule za kiafrika.
  • Habari za elimu za kiafrika kwenye mtandao wa kompyuta.
  • Tumafanyakazi kuelekea kwenye uendelezi wa yaliyomo kwenye mtandao kwa kutumia lugha za wenyeji

Sisi ni nani?

 

SchoolNet Africa inafanya kazi na viongozi  wa miradi ya SchoolNet Africa katika nchi zisizopungua thelathini za kiafrika.

  • Angola
  • Benin
  • Botswana
  • Cameroon
  • Cape Verde
  • Ivory coast
  • Misri
  • Ethiopia
  • Gambia
  • Ghana
  • Kenya
  • Lesotho
  • Malawi
  • Mauritius
  • Morocco
  • Msumbiji
  • Namibia
  • Nigeria
  • Rwanda
  • Senegal
  • Sierra Leone
  • Swaziland
  • Tanzania
  • Uganda
  • Zambia
  • Zimbabwe

 

Historia yetu

Hii yote ilianza kwenye warsha iliyofanyika Cape Town mwezi wa tisa, 2020 ambapo ilihudhuriwa na wawakilishi wa SchoolNet kutoka nchi kuni za kiafrika. SchoolNet Tamko la hali ya Afrika ambalo lilikuwa limepangwa kwenye makala ya maendeleo ya uchumi ya Afrika (ADF) yaliyodhaminiwa na kamati ya umoja wa mataifa ya maendeleo ya uchumi wa Afrika (UNECA) mwezi wa kumi na moja ’99, yalikubaliwa katika warsha hii. ADF kwa utaratibu walikubali jitihada zetu.

Tazama: Ripoti ya SchoolNet  Cape Town. Kwa habari zaidi kuhusu hatua hii.

Kwa msaada kutoka kituo cha kimataifa cha utafiti wa maendeleo ( IDRC), mpango wa biashara wa SchoolNet ulioandaliwa na kupangwa kwenye warsha ya mitandao ya shule katika Afrika, iliyofanyika Okahandja, Namibia mwezi wa saba mwaka 2020. Warsha hii ilidhaminiwa na SchoolNet Namibia, Wizara ya elimu ya Namibia,, Taasisi ya Taifa ya maendeleo ya Elimu na IDRC. Ilihudhuriwa na wawakilishi zaidi ya 100 kutoka kwenye miradi ya SchoolNet, wiraza za Elimu, mashirika binafsi kutoka nchi ishirini za kiafrika. Hapa kamati ya muda ya uongozi ilichaguliwa kukiwa na wawakilishi wawili kutoka katika kila maeneo matano ya Afrika.

Tazama: Ripoti ya warsha ya SchoolNet Africa.

Kwahabari zaidi:

Mwezi wa saba 2020 kamati ya uongozi ya muda ilikutana kwa mara ya kwanza huko Cape Town na kuendelea kuanzisha SchoolNet Afrika kama asasi inayojitegemea ikishirikiana na taasisi ya jamii huru ya kusini mwa Afrika (OSISA).

SchoolNet Africa ulizinduliwa rasmi tarehe 12 November 2020 .