Feedback Sitemap Send page Print Help
Watoto waliopigana vita

Vita vinaendelea kkuharibu nchi za kiafrika ikiendelea kuwanyima vijana haki zao za msingi na kuzuia malengo ya elimu kwa wote katika Afrika.

Watoto waliopigana vita wanajikuta bila kuwa na sauti, wametengwa na hivyo wanahitaji kusaidiwa kuweza kurudi kwenye jamii. Kwenye kipengele hiki  tunakupatia tovuti za mawakala ambao wanahusika na urekebishaji na uelimishaji wa watoto waliopigana. Pia utapata vitu ambavyo vitakuonyesha ni jinsi gani ICT. Zinaweza kutumika kama kichocheo kwenye kurahisisha elimu na mawasiliano kati ya wototo wapiganaji.

Ujumbe kwa wafadhili:

SchoolNet Afrika inawataka washika dau wote wa elimu katika Angola, Liberia na Rwanda, asasi zisizo za serikali (NGOs) na jumuiya ya wafadhili kusaidia mradi wetu, kutoka kwenye bunduki kwenda kwenye kompyuta. Tunatumaini kwmaba kufanikiwa kwa mradi huu wa majaribio kutaongoza kwenye upanuzi wa nafasi za elimu kupitia ICTs kwa watoto waliopigana katika nchi zilizoathirika kwa vita.

Makala

Elimu katika Nyenzo za dharura - 2020 Aug 25
Nyenzo hizi kimsingi zinalenga wafanyakaszi wanaohusika na kuanzisha na kuogoza miradi ya elimu katika kipindi cha mpito. Inaweza kuwa pia ya manufaa kwa wale wanaoongoza vikundi vya dharura, au wale wanaoandika mapendekezo, kuandaa na kuendesha mchanganuo.

Nyenzo

Kujifunza kwa wakati ujao: Elimu ya wakimbizi katika nchi zinazoendelea:
Inaangalia elimu kama njia ya kujenga maisha ya watoto wakimbizi, kupitia ushirikiano wa kijamii na kupata maarifa na ujuzi kwa maisha yao ya baadaye. [510]
http://www.unhcr.ch/pubs/epau/learningfuture/learningtoc.htm

Schools Demining Schools
Schools Demining Schools ni mradi wa vitendo ambao si tu utajifunza kujadili na kuchapisha bali utachangia kwa kiasi kikubwa kutatua moja ya matatizo ya kutisha ya wakati wetu; tatizo la mabomu ya kutegwa ardhini. [509]
http://www.un.org/cyberschoolbus/banmines/about/whatis.asp

IEARN: Sierra Leone
Lengo la IEARN Sierra Leone ni kuwarekebisha vijana ambao wamepata ugumu kutoka katika vita madhara ya vita. Kutumia kompyuta na mtandao, walimu wanasaidia kuunda ICT na ujuzi na mawasiliano kwa vijana hawa wakiwa na malengo ya kuwa raia wema. [508]
http://www.iearnsierraleone.org/

Mtandao wa kimataifa wa LifeLine
Kama matokeo ya uzoefu uliowaumiza wakati wa vita virefu vya umwagaji damu katika vita vya Siera Leone, maelfu ya watoto wameathirika. Mwaka ’96 Sierra Leone iliwaalika LifeLine West Africa Ministries (sasa inajulikana kama LifeLine Development Organization) kwa kushirikiana na LifeLine Network International (LNI) kuanzisha mradi wa marekebisho kwa watoto hawa. [507]
http://www.thenehemiahproject.org