Feedback Sitemap Send page Print Help
Uboreshaji wa elimu

Makala

Uzuiaji wa Internet kwenye shule za umma - 2020 Aug 19
Electronic Frontier Foundation (EFF) na Online Policy Group (OPG) wameshirikiana kujifunza na kuandaa upatikanaji wa tovuti zinazohusiana na habari za mitaala ambayo ni lazima kwa taifa katika shule za umma ambayo inaendesha uzuiaji wa vifaa vya mtandao wa internet. Makala hii inapima kwa kiwango ambacho uzuiaji wa vifaa vya kompyuta inaadhiri maendeleo ya elimu kwa kuzuia upatikanaji wa tovuti zinazofaa na zinazohitajika katika mtaala.

INTEL - 2020 Jun 30
Mkutano wa umoja wa mataifa wa teknolojia ya habari na mawasiliano na nguvu kazi (UNICT).

SchoolNet Namibia inatumia ufumbuzi wa mawasiliano bila waya - 2020 Jun 10
Karibu theluthi mbili za shule za Namibia bado hazina mawasiliano ya simu, lakini hilo halitawazuia kuweza kupata huduma ya mtandao wa kompyuta. Ujenzi umeanza wa kusambaza mtandao wa internet bila kutumia nyaya au njia ya simu.

Nyenzo

Sauti kwa masomo ya mbali na ujifunzaji wazi
Kitabu hiki kinalenga kutoa wataalam wazuri katika tabia ya ubunifu, uendelezaji na upelekaji wa vifaa vya sauti (redio, kanda na kanda za picha) kwa mafunzo wazi na ya mbali. [664]
http://www.col.org/audiohandbook/audiohandbook.htm

Safari ya haraka kwenye darasa la linux
Tumekuwa tukitumia linux kwa miaka miwili sasa kwa madarasa ya 4-8. Tungependa uone ni jinsi gani K12 linux inavyofanya kazi. [661]
http://www.k12ltsp.org/classroom.html

Kuchanganya na kuoanisha vifaa vya elimu ya mbali
Kwa mara ya kwanza, kuibuka kwa viwango vya vifaa vya kompyuta vinawezesha vyuo kumudu mipango ya mafunzo ya mbali kwa kuchanganya mafunzo ya kwenye kompyuta na vifaa vya kompyuta vya kampuni mbali mbali. Dazeni za vyuo duniani kote wanashiriki kwenye uundaji wa viwango vipya, mamia ya taasisi, mashirika na vyombo vya serikali tayari wanavitumia. [660]
http://chronicle.com/free/v48/i37/37a20201.htm

Kamusi mpya ya IT iliyoandaliwa Benin
Watafiti wa Benin wamechapisha kamusi mpya ya teknolojia ya mawasiliano na habari (NICT). Kulingana na mwandishi wake, Dr. Daouda Abdou Razak, miaka saba ya utafiti iliwekwa pamoja. Kamusi hiyo ni ya lugha mbili (kifaransa-kiingereza). [659]
http://www.h2com.com/lematinal/Archives/202014/mlpolitique9.htm

Kutengeneza maktaba yenye vyanzo vya vifaa vya kompyuta vilivyo wazi
Maendeleo na ushirikianaji wa maktaba ya vifaa vya kompyuta vitapatikana katika maktaba ya vifaa vya kompyuta ya Green Stone Digital Library ambayo itasaidiwa na UNESCO itakayoendesha mafunzo katika warsha ya wajifunzaji wa Asia katika Mai, katika kituo cha teknolojia ya hali ya juu cha India kilichopo Bangalore. [658]
http://www.k12handhelds.com

Radio hufundisha kiingereza kwa watu wa vijijini Afrika Kusini
Asasi za elimu za Afrika Kusini zinatumia njia ya redio kufundisha kiingereza kama lugha ya pili. Mpango wa kufundisha kiingereza kwa redio ni njia za ushiriki, ambazo ni mpya kwa walimu wengi na hufika sehemu ambazo njia nyingine haziwezi kufika. [657]
http://www.sn.apc.org/olset/targetgr.htm