Feedback Sitemap Send page Print Help
Mradi wa Vijana Duniani

Hebu fikiri jinsi  ambavyo masomo/kujifunza kungekuwa endapo wanafunzi na waalimu wangeingia kwenye mtandao mara kwa mara na kujadilina hoja kama misitu (katika maeneo yenye mvua nyingi)  huko Bolivia au athari za utandawazi au athari za gonjwa la UKIMWI na wanafunzi waliopo Ghana na Surinam.

 

Mradi wa Vijana Duniani  tayari umekwishabadilisha ndoto hii na kuifanya kuwa ukweli wa kila siku   wa wanafunzi 3000 kutoka nchi 20, na shule nyingine huomba kujiunga siku hadi siku. Tangu ulipozinduliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2020, Mradi wa Vijana Duniani(MVD) umepanuka kutaka shule 3 za sekondari hadi kufikia shule 105. Matokeo ni kupanuka kwa mtandao wa kufikirika wa shule za sekondari unaokuwa kwa kasi katika nchi zinazoendelea (maskini) na zile zilizoendelea(tajiri) pamoja na kizazi chenye watu wenye mwelekeo katika habari, elimu na ufahamu wa tamaduni mbalimbali.  

                            

Dhumuni

Madhumuni ya mtandao huu yapo katika sehemu mbili:

Kustawisha ubora  wa  elimu ya sekondari kwa kuziingiza shule hizi katika matumizi mapya (yaliyopo) ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(ICT)- vyombo vya habari; na,  kustawisha ufahamu miongoni mwa tamaduni mbalimbali na upeo kwa kuanzisha midahalo ya mara kwa kwa mara madarasani, katika mazingira salama na yenye mwelekeo, yanayojumuisha wanafunzi wa shule za  sekondari kutoka sehemu mbalimbali za dunia.

 Midahalo wakati wa shughuli halisi, mzunguko wa vipindi, hufanyika katika mazingira ya chuo cha kufikirika, ambayo hufananishwa na mazingira ya chuo kikuu halisi, mahali penye mawasiliano kwa njia ya mtandao. Kwa njia hii, Mradi wa Vijana Duniani unaleta mageuzi kabisa katika njia ya ufundishaji madarasani.

Sababu za Mafanikio

Mafanikio ya huu mradi yanatokana na urahisi wake. Huziandalia shule kifurushi(programu) cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano    kilichohakikiwa na kujaribiwa, chenye gharama nafuu, na chenye kutosheleza kwa urahisi. Pia  hudumu. Hii hutokana na ukweli kwamba mradi unamilikiwa kienyeji:

Kila mhusika wa huu Mradi anachukuliwa kama mshika dau kama ilivyo kwa   wengine. Taarifa kutoka kwa wahusika husisitizwa sana, ambayo huwawezesha maofisa(wawili) wa Mradi kuboresha na kuufanya mradi kuwa safi.

Manmo mwaka 2020, IICD na MediaPlaza walianzisha jumuiya kwa ajili ya kumbukumbu ya hayati Johan Kooij, Mreno aliyekuwa na imani thabiti juu ya nguvu ya elimu katika kuunganisha watu. Jumiya hii huwapatia wasimamizi wa mradi katika nchi husika tukio fulani  kuhusiana na mtandao huu kila mwaka, mahali fulani duniani. Mpaka sasa kuna wasimamizi   20 (ngazi ya taifa) wa IICD walioteuliwa ambao hutoa msaada endelevu na muongozo kwa shule zote zilizopo kwenye mradi, waalimu na wanafunzi katika nchi zao.

Shughuli za Mradi

Kuna shughuli kadhaa katika Mradi wa Vijana Duniani, ikiwa ni pamoja na mzunguko wa vipindi. Huanzia miradi ya pamoja, semina za pamoja, mikutano na mazungumzo.

Jinsi ya Kujiunga

Kama ungependa kujiunga na mradi, tafadhali wasiliana na mmoja wa maofisa wa Mradi moja kwa moja kwa kutumia anwani ya barua pepe au namba ya simu hapo chini. Endapo kuna shule nyingine katika nchi yako tayari zinajihusisha na mradi, tutakuunganisha na msimamizi wa mradi katika nchi yako. Barua pepe: [email protected]

For more information, see http://www.iicd.org/globalteenager/

Kwa habari zaidi, tazama: http://www.iicd.org/globalteenager/