Feedback Sitemap Send page Print Help
Mitandao ya jinsia
Nyenzo

Mfuko wa dunia wa elimu ya wasichana
GGEF ni tofauti sana kwa kuwa ni taasisi pekee ambayo lengo lake ni kupeleka wasichana pekee shule. Kuonyesha pengo lililopo kati ya wasichana na wavulana katika elimu, wanataka kuwapa wasichana mipango yao wenyewe. [633]
http://www.ggef.org

Mfumo wa kusimamia elimu ya msichana
Mfumo wa kusimamia elimu ya msichana ni semina iliyofanyika nchini Mali. Makala hii inaeleza kwa ufupi maendeleo ya mtizamo wa mradi wa SAGE/Mali unaofadhiliwa na USAID. Miaka miwili na nusu ya mradi huu unaangaliwa kwa uhusiano wa mfumo wa miundo mbinu ya elimu kwa msichana na wanawake wa SAID/EGAT/WID ambao SAGE/Mali ni sehemu ya mradi huu. [632]
http://www.educategirls.com/

Okoa watoto
Kuna ufikiwaji tofauti kwa kuwekeza kwenye elimu ya wasichana. Mfano wa awali kutoka “save the children”(SC) katika Mangochi, Malawi ni mmojawapo kati ya mingi inayoonyesha jinsi asasi zisizo za kiserikali (NGOs) zinavyosaidia katika jitihada za elimu ya msichana na kusaidia kutambua umuhimu wa elimu kwa wote. SC inafanya hivi kwa ushirikiano na jamii zenyewe, NGOs na wizara za serikali duniani kote. [631]
http://www.savethechildren.org

Msaada wa jamii kwa elimu ya msichana
Msaada wa jamii kwa elimu ya msichana (CAGE) ni mradi wa majaribio wenye miaka 2 uliobuniwa ili kurahisisha shughuli za jamii ili kumsaidia msichana katika elimu na kuinua ushiriki wa wasichana wa vijijini huko Benin kwa kuondoa na kuharibu vikwazo kwenye mafanikio ya kusoma yanayotokea nje ya shule na madarasa. [629]
http://www.worldlearning.org/wlid/proj_benin_cage.html

INSTRAW
INSTRAW inafanya kazi kuelekea kwenye usawa wa jinsia na kuwatia nguvu wanawake kupitia GAINS (Gender Awareness Information and Networking Systems), utafiti unaofanyika kwenye mtandao wa Internet na mazingira ya mafunzo yanayoendeshwa na mtandao wa dunia nzima. Kwa kurahisisha kazi za ushirikiano inataka kuunda na kushirikiana maarifa kuboresha maendeleo ya sera na utekelezaji. [628]
http://www.un-instraw.org/

FAWE
Forum for African Women Educationalist (FAWE) uliundwa mwaka ’92 kufuatia maendeleo ya polepole ya utekelezaji wa malengo yote ya elimu katika nchi zilizo nje ya Sahara. [627]
http://www.fawe.org/

Mtandao wa wanawake
Mtandao wa wanawake ni mtandao mzuri na hai uliobuniwa ili kuwawezesha wanawake wa Afrika ya Kusini kuweza kutumia Internet kutafuta watu, habari, vyanzo na nyenzo zinazohitajika katika ushiriki wa wanawake kijamii. [626]
http://www.womensnet.org.za

WSIS Gender Caucus
WSIS Gender Caucus inajumuisha wawakilishi wa asasi ambazo zilikubali mwaliko wa UNIFEM kuchangia katika kuhakikisha kwamba nafasi ya jinsia inajumuishwa katika hatua za kuelezea na kuunda jumuiya ya habari duniani ambayo inachangia kwenye maendeleo endelevu na ulinzi wa mwanadamu. [625]
http://www.wougnet.org/WSIS/wsisgc.html